Kenya 🇰🇪 Teachers Are The Most Well Paid In East Africa

Image
ANALYSIS By Dorris Otieno Kenyan teachers are not only the best paid in East Africa, but also earn almost 12 times more than the country's average pay, a comparative study by Nation Newsplex and the Institute of Economic Affairs reveals. Even as teachers go on strike for the 12th time since their first industrial action in 1962, the analysis, which compares teachers' salaries in Kenya with those of their peers in select African countries , also finds that the lowest-paid teacher in Kenya earns more than the highest-paid teacher in Uganda. Uganda and South Africa were chosen as countries against which to compare wages of teachers because they have the most up-to-date data against which the comparison could be made. While Tanzania was not included in the comparison because only average pay for the year 2011 was available, even its figures indicated that Kenyan teachers earn more than their Tanzanian counterparts. The highest paid Kenyan teacher earns almost 12 times more than the

MBINU SABA (7) KUONGEZA WAFUASI KATIKA INSTAGRAM




MBINU SABA KUONGEZA WAFUASI KATIKA INSTAGRAM

Tangu kuanzishwa kwake Instagram imekuwa mstari wa mbele na matumizi mengi kutoka kwa vijana na watu wenye umri wa kati.
Instagram imekuwa mtandao unaokua kwa kasi sana kuliko Mitandao mingine. Na utafiti umefanyika kuonyesha kuwa watu wenye umri kati ya miaka 20-60 wanautumia hivyo kama una mashaka kuwa uwezi kuongeza Wateja kupitia Mtandao huu umekosea!


Sasa ni kweli kuwa watafuta masoko mtandao hawatumii Mtandao huu kutafuta Wateja? Kipindi cha nyuma kinaonyesha kulikuwepo mtazamo usio wa uelewa (uncognitive bias) linapokuja suala la kuuza kupitia Instagram. Instagram imeanza kutumia na kuunganisha akaunti yako na Wovuti kwenye "bio" katika sehemu ya maelezo binafsi "profile". Hivi ni viashiria kuwa Instagram ni Mtandao Maudhui Masoko ( Content based platform) ambao uwezi kupata matokeo mazuri ya uwekezaji ( Return On Investment, ROI). Lakini hii ni upotoshaji, kwani kila Mtandao una namna yake ya kutafuta masoko. Mara nyingi watu upenda kujaribu kutumia kila Mtandao kutangaza bidhaa zao. Kama utajaribu kutumia njia moja kwa kila mtandao kama Facebook, Twitter, na Instagram, itakusaidia kuokoa muda na nguvu unayotumia. Hii itakusaidia kuwepo katika kila mtandao na kufanya upate Wafuasi wengi na kukuza biashara yako. Lakini Mitandao ya Kijamii umuhimu wake haupo kwenye kuwa na wafuasi wengi lakini upo kwa namna gani unajihusisha na hao wafuasi kwa kutumia mtazamo wa kila saiti. Kama utaitumia Instagram jinsi unavyotumia Barua Pepe au Twitter ni wazi biashara yako haitapata matokeo mazuri ya Wateja kwani mbinu ya Instagram ya kutumia picha ni tofauti na Mitandao mingine. Watumiaji wake wamezoea matumizi ya picha, jambo linalochukua muda mwingi kuilewa positi (post). Ukitaka kuwa na wafuasi wengi katika Instagram unahitaji kuwa karibu nao. Ikiwa na watumiaji karibia 800 millioni, itakubidi uwe mwangalifu kutumia. Lazima uonyeshe uhalisia wa bidhaa yako, na manufaa yapatikanayo kutoka kwa huduma utoayo.

Mbinu 7 kuongeza mawasiliano kwenye Instagram:

1) Jenga Portfolio (Build A Portfolio):

Kabla ya kuanza kujenga msingi wa wapenzi wako lazima utoe maelezo yako binafsi ( profile) ambayo yapo wazi kwa kila mtu ( public). Kwenda kwenye "Settings” kwenye mkono wa kulia wa kioo chako na hakikisha alama ya “Private Account” haiwaki.
Baada ya Akaunti yako kuwa inaonekana kwa umma basi unaanza kupost na kumbuka hakuna anayetaka kumfuata mtu mwenye picha chache za kuonesha. Kama unataka kutambuliwa basi tayari uwe na picha kati ya 20-25 zenye mvuto. Kama unatumia simu aina ya iPhone, kuna njia za kutengeneza picha zenye mvuto (quality). Hakikisha fotos zako zinaeleweka kwa Wateja wako mfano kama biashara yako ni kuuza viatu basi onesha viatu ambavyo Wateja wako watapenda.
Kila picha, andika maelezo mafupi yanayoeleza kwa ufasaha picha uliyoweka ambayo itahamasisha mtu kukufuata.
Kabla ya kuweka picha, tumia hashtags zinazohusiana na picha zako, na ambazo zitatangaza bidhaa zako mbele ya watu wengine.


2) Sambaza na Kukuza Akaunti zako katika Mitandao ya Kijamii:
 
(Cross-Promote Your Social Profiles)

Unahimizwa kuanzisha akaunti zenye kukueleza wewe binafsi kwenye Mitandao mbalimbali ya Kijamii na kama kuna umuhimu huo kwa nini basi hivyo hivyo akaunti yako ya Instagram nayo uache kuitangaza na kuipa kipaumbele? Instagram inaruhusu kutuma na kutangaza picha kwenda Facebook. Sasa kwa nini usiwaombe fans wako wa Facebook wasikufute vilevile uko Instagram? Unaweza kutumia mkakati huo huo kwenye Twitter na LinkedIn. Kumbuka unataka kupata wafuasi na siyo kuwapoteza. Omba mitandao yote wakufuate kwenye Instagram matokea yake utayaona kwa muda mfupi.
Mkazo uweke katika kutangaza Mtandao mmoja baada ya mwingine bila kuchanganya Mitandao mingi kwa wakati mmoja!


3) Jitanue kwenye Hadhira yako: kwenye Mitandao ya Kijamii, kwani kila eneo lina mamlaka yake kitakwimu. 

Katika hili bila kujali ushawishi wako uko ,siku zote kutakuwa na watu wanasubiri kupata mfuasi na kwako pia unahitaji mtu aliyeko tayari kukupokea.
Kama unataka kujijengea umaarufu wa kudumu Instagram, basi inahitaji kujiunganisha na watumiaji wengine na kuwaomba na kuwahimiza ili wakutangaze ndani na nje ya Mitandao mingine mingi.


4) Kujihusisha na wafuasi wako:

Kwa bahati mbaya, watu wengi uweka mtazamo juu ya Kipengele cha UCHUMBA (ENGAGEMENT)kwa wafuasi. Hakuna haja ya kuingia Instagram na kupata wafuasi wengi kama uweki juhudi kujenga mahusiano nao.Hatua ya kwanza ni kujenga maudhui na kulazimisha mahusiano yenye msingi thabiti. Hutaki wafuasi wako kusahau wewe ni nani!
Kama utaingia kwenye Mitandao ya Kijamii kupata wafuasi wengi utajikuta upo pekee yako lakini ukiingia na kujenga mahusiano kwanza utashangaa wanaongezeka kila kunakokucha bila kitumia nguvu kubwa. Chukua muda kujibu maswali ya wafuasi wako na hii itakutabainisha na watu wengine kwenye Instagram.
Wafuasi wako wanapoona unajihusisha nao kunaongeza nafasi zao kushare na kukomenti kwenye picha unazotuma. Jibu dogo la "AHSANTE" litaongeza furaha na kuridhika kwa mfuasi wako. Kumbuka lengo lako ni kuwa na wafuasi wenye hamasa kwako ambao utawageuza kuwa Wateja wako wa kudumu wa kununua bidhaa zako!


5) UBORA WA MAUDHUI dhidi ya WINGI:

Uwezi kutegemea kupata mwingiliano mkubwa kutoka kwa watumiaji kama utatuma picha kiduchu ndani ya wiki. Pia, huhitaji kufanya mafuriko ya picha kwa muda mfupi. Hivyo, lazima upime na inashauriwa kutuma picha moja kila baada ya masaa 3-4
Jambo la kukumbuka muda wote ni kuwa tanguliza #UBORA vs #WINGI wa PICHA. Badala ya kujali wingi wa picha unazotuma, chukua muda kuelewa picha zinazowavutia wafuasi wako kwani ni vema kutuma picha zenye mvuto na maudhui tamu ata kama chache kuliko kutuma nyingi zisizovutia kabisa.


6) Tuma Picha zako Wakati Muafaka:

Kama utataka kupandisha chati ya mahusiano na wafuasi wako unatakiwa kutuma picha kwa Wakati Muafaka. Hii utaona ni kichekesho lakini unapashwa kuwajua wafuasi wako kiundani sana nakujua muda mzuri wa kupost kwenye Mitandao ya Kijamii.
Kuliko kutegemea takwimu za kupewa fanya utafiti wako mpaka ujue muda ambao kwenye eneo lako watu wengi wanatumia Instagram kusudi unapotuma picha yako ionwe na watu wengi na kuongeza muingiliano wa kutosha.


7) Taja "Link kwenye Bio"

Kama nilivyotaja awali Instagram inakataza kuweka "link" ,zinazotoka kwenye picha hivyo ni jukumu lako kumjulisha msomaji wako mahali pa kupata maelezo marefu ya picha uliyotuma kwenye bio ambayo itakuwa link ya blog yako unayotumia.
Hii itakusaidia kuiunganisha blog yako na kutengeneza list ya barua pepe kupitia Instagram na kupata watumiaji wengi wa bidhaa zako ( Subscribers)


Hitimisho
 
Instagram ina njia ya kipekee ya kuwafikia watumiaji wake kwa kutumia picha, foto au michoro na imebadilisha Tabia na matumizi ya Mitandao ya Kijamii kwa muda mfupi na inavyozidi kukuwa na kupata umaarufu kwa watumiaji wa Rika mbali mbali ndivyo inavyozidi kuhitajika kwa wana Mkakati Maudhui Masoko. Utakuwa unafanya kosa kudhani kuwa Wateja wako hawaitumii Instagram kabla hawajaamua wanunue wapi mahitaji yao.

Ni jukumu lako sasa kuzielewa mbinu hizi kama unataka kuitumia Instagram kuongeza mapato ya biashara yako.



Comments

Popular posts from this blog

LinkedIn: A Social Networking Site for Business People and Professionals To Connect

The Tanzania Government Invites You To Discover Some Compelling Reasons To Invest.

Investment Opportunities in Integrated Waste Management in Tanzania