Kulingana na Utafiti uliofanywa na "Creative Group", 50% ya
Maafisa Masoko kwenye Makampuni walisema wanategemea kuongeza uwekezaji
Facebook mwaka huu.
Facebook ni rahisi, unaboresha ukurasa wako wafuasi
watafurika haraka sana na kujibu! Hiyo ni ndoto ya kila mwenye kuingia
hapa kabla hajaanza au ndivyo alivyosikia kutoka kwa watu wanaodai ni
Wataalamu katika fani hii. Wengi wao uishia Kutelekeza Kurasa au kuacha
wasipoona matokea mazuri wanayotarajia licha ya kutuma taarifa mara kwa
mara! Hapa nikupe ukweli; watu hawahitaji kusikia au kuona bidhaa yako
mara kwa mara. Kwa nini wasikie au waone wakati muda wote wanakuwa
wamerundikiwa na Matangazo kutoka Mbaoni, TV, Radio ata mtu
anapotembelea mtandao wa Inteneti. Ngoja tukabiliane na ukweli huu; watu
hawaji Facebook kuona matangazo. Kinachowaogopesha wenye kutangaza ni
kuwa Facebook imetengenezwa ikimpa mtumiaji nguvu ya kutawala, hivyo
anaweza kuamua kulidharau na kuliacha kando Tangazo lako akiamua kufanya
hivyo. Kuongeza mahusiano mazuri Facebook unahitajika kuandika vitu
vyenye maudhui matamu na vya kipekee.
Kulingana na Uzoefu nilionao na kutumia wengine walionitangulia katika
fani hii, nitakupa njia zilizonisaidia kuongeza mahusiano kwenye Ukurasa
wangu na nilichoona kimewasaidia wenzangu.
1. Uliza Maswali
Maswali ni njia muhimu ya kuchochea mazungumzo na washabiki wako. Uenda
ndio njia rahisi ya kuwafanya watu wajihusishe na unachokituma. Kuna
maswali mengi ya kuweza kuwauliza washabiki wako,
2. Muda wa Kutuma
Muda wa kutuma "posts" ni muhimu sana kwenye Mitandao ya Kijamii.
Fikiria unatuma ujumbe muda ambao kila mtu yupo kazini au yupo
usingizini . Ni vema kutuma ujumbe wakati watu wamemaliza kazi au wapo
kwenye usafiri wanarudi nyumbani. Hizi ndizo nyakati watu utembelea
akaunti zao kwenye mitandao ya kijamii kuona kinachotumwa na wenzao.
Kulingana na Dan Zarella, muda mzuri wa kutuma post kwenye Facebook ni
mchana na muda kidogo kuanzia SAA 1 Jioni.
3. Picha
Tunaambiwa kuwa Picha uwakilisha maneno elfu, kweli? Kwenye Facebook
Picha ina maana zaidi ya maneno elfu moja. Picha lazima zitumiwe
kurahisisha mawasiliano na mahusiano kwani usimamia vizuri kuliko Jumbe
nyingine au links. Picha uwa wazi na fupi na rahisi kueleweka. Leneys,
kampuni ya mitindo kwa akina mama utuma Picha nyingi na kuwaomba
washabiki kuchagua mitindo wapendayo. Matokeo yake ni makubwa. Post hii
tu iliwapa 51 komenti, 52 likes na 55 shares kutoka kwa fans na
wakiwaomba marafiki wao wasambaze na kushirikisha wengine!
4. Mashindano ya Facebook
Mashindano ni njia muhimu ya kuongeza mahusiano kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook
kwa sababu siyo tu inawazawadia wafuasi watiifu lakini inaleta hamasa
kwa watumiaji kutembelea Ukurasa wako mara kwa mara ili kuona kama
wameshinda. Kuna mashindano ya aina nyingi unaweza kuendesha. Matangazo
katika Mitandao ya Kijamii, mfano, Binkd, siyo tu yanaruhusu kujenga
shindano la ukweli na uwazi, lakini yanaleta changamoto kwenye kujenga
mahusiano. Mashindano tofauti yanaweza kukusaidia kulenga mahusiano
utakayohitaji kutoka kwa hadhira na watu unaowahitaji. Mashindano ya
'Kura ili Ushinde' yatakuletea 'likes' nyingi, lakini siyo komenti
nyingi kama mashindano mengi yenye kuleta changamoto kubwa yatakufanya
uandike tagline kwenye kisanduku cha kutoa maoni. Mari Smith siku za
karibuni aliendesha Shindano lililofanikiwa kwa kutumia Strutta.
Shindano lake lilipata ingizo zaidi ya 392 kutoka kwenye washiriki
maalum 377. Shindano lake pia liliingiza kura 15,571 kutoka kwenye
wapiga kura maalum 2,153. Moja ya Ujumbe wake alioutuma kwenye
shindano ulipata zaidi ya ushirikishaji 50, maoni 42 na liki 150 na
hiyo ni positi moja tu!
5. Majibu kwa Kutumia "Crowdsource"
Kuliko ujibu maswali mwenyewe , kwa nini husitumie Marafiki wako
wawasaidie wengine wanaohitaji maelekezo na ushauri? Hivyo ndivyo
Natural Parenting Tips, Ukurasa wa Facebook ambao umejitoa kuwasaidia
Wazazi/Walezi unafanya. Kila siku bila kuacha uuisha ukurasa na maswali
kutoka kwa marafiki. Wazo hapa ni kutumia Crowdsource kwa vidokezo
kutoka kwa Wafuasi wako,ambao husaidia kushauri wengine.
6.Wito kwa Vitendo
Wito
kwa Vitendo unawawezesha wanamasoko mtandao kisaikolojia kuwatumia
Wafuasi wao kwa namna wanavyotaka. Kitu tunachokosea mara kwa mara ni
kusahau kuuisha WITO KWA VITENDO ( CALL TO ACTION) kwenye Kurasa zetu za
Facebook. Hadhara yako uwa inaitikia vizuri kama imeelekezwa namna ya
kuitikia.Unataka watu wafanye nini? Watoe maoni gani? Wabonyeza kifungo?
Washiriki jambo na wenzao? Subway, kampuni ya kimarekani inajua vizuri
maana ya WITO WA VITENDO! Kila mara kwenye ukurasa utakuta wanawaelekeza
wateja kitu cha kufanya, Mfano like hapa, washirikishe wenzako,
Bonyeza, hii pekee iliwasaidia kupata Likes 53,000 na shares 404.
7..Matangazo ya Facebook
Ukiona namba ndogo ya watu ndiyo inatembelea Ukurasa wako,nini utafanya
kuongeza namba inayotembelea ni kuanza na Tangazo la Facebook. Hii
inasadia kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi
8. Mpangilio wa Kutuma Ujumbe ( Frequency Of Posting)
Mpangilio
wa kutuma positi zako nao una maana kwenye Mahusiano na Washiriki wako
Facebook. Tukirejea kwenye Utafiti wa Buddy Media, Kurasa ambazo uwa
zinatuma Ujumbe mara mbili kwa siku upata 40% ya mahusiano ya juu kuliko
wale wanaotuma mara 3 au zaidi kwa siku. Hii inaonyesha kuwa
kinachomata siyo Idadi bali Ubora wa kinachotumwa Facebook. Jambo moja
linaweza leta mafanikio kwa mtu mmoja na si lazima liwe hivyo kwa kila
mtu.Unahimizwa kujaribu njia hizi ili uone ni ipi inafanya kazi kuliko
nyingine
Comments