Kenya 🇰🇪 Teachers Are The Most Well Paid In East Africa

Image
ANALYSIS By Dorris Otieno Kenyan teachers are not only the best paid in East Africa, but also earn almost 12 times more than the country's average pay, a comparative study by Nation Newsplex and the Institute of Economic Affairs reveals. Even as teachers go on strike for the 12th time since their first industrial action in 1962, the analysis, which compares teachers' salaries in Kenya with those of their peers in select African countries , also finds that the lowest-paid teacher in Kenya earns more than the highest-paid teacher in Uganda. Uganda and South Africa were chosen as countries against which to compare wages of teachers because they have the most up-to-date data against which the comparison could be made. While Tanzania was not included in the comparison because only average pay for the year 2011 was available, even its figures indicated that Kenyan teachers earn more than their Tanzanian counterparts. The highest paid Kenyan teacher earns almost 12 times more than the

Namna ya Kutumia WhatsApp Kibiashara





Nimeona leo niwahusishe na kuwaletea somo moja la “NAMNA YA KUTUMIA WHATSAPP KIBIASHARA”. Nyote ni mashaidi kuwa linapokuja suala la mitandao ya kijamii, WHATSAPPimetokea kuwa na matumizi makubwa kutokana na mfumo wa kutumia UJUMBE kutoka kwa mtu kwenda kwa mwingine (personalized messages).

Hii inaufanya mtandao huu wa Kijamii kwa sasa kuwa maarufu katika Ulimwengu wa Digitali na unatumika kama kifaa cha kuendeleza biashara hasa suala la utafutaji wa MASOKO NA FURSA.

Namna ya Kutumia WhatsApp

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2014 uko India, WhatsApp ilitumiwa kwa wingi na nguvu na Vyama vya Kisiasa kama chombo cha kuwafikia wapiga kura kwa urahisi. Matokeo yalikuwa makubwa,kwa Vyama Vya Siasa kupeleka Ujumbe wa kuelezea SERA zao kwa wananchi kwa haraka na muda mfupi.

Nipende kusema siyo Wanasiasa tu wa India lakini hata hapa Nchini kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, tumejionea jinsi habari za Uchaguzi na Kampeni kutoka kwa Wagombea zilivyo kuwa zinatufikia kwa urahisi kupitia WhatsApp.

Mkakati huu wa kujitangaza kwa Wafanyabiashara, Watoa Huduma, unatumiwa sana na wataalamu wa masoko kijiditali ( Digital Marketing Experts) kwa kutumia umaarufu wa WHASAPP na kukigeuza kama chombo cha KIMKAKATI CHA KUTAFUTA MASOKO(effective social media marketing tool).


Nani Ujiunganishe naye?

Kwanza katika shuguli yako unayofanya uwe Mkulima wa Nyanya, Vitunguu,uwe Muuza Duka, Mfugaji, Fundi Ujenzi, Fundi wa Mbao,Msafirishaji,  Mwenye Salon, Kiwanda cha Juisi, au Mtoa Huduma ya Afya na Shule, Wakala wa Bima, Mama/Baba Ntilie, Muuza Genge, Baa, Nyumba ya Kulala Wageni na Hoteli, Mvuvi, Mrina Asali, Mtoa Huduma za Kifedha kama Vicoba, Saccos na Benki, NGO na Mwanasiasa ni lazima ujiunganishe na Wateja wako ulionao na unaowajua tayari. Muunganiko huo utasaidia kujenga maelewano zaidi na wateja wako.

Kwa kuwa wateja awa tayari wametumia bidhaa au huduma yako, watakuwa wazi kukubali bidhaa au huduma mpya utakayoileta sokoni. Kutuma Ujumbe wa kupromoti kwa kila mtu halimradi unaweza kuleta matokeo hasi kwa bidhaa au huduma unayotangaza tofauti na kama utalenga kwa wale wateja ambao uliwai kuwahudumia.

Makundi ya WhatsApp ( WhatsApp Groups)

Zao kubwa la WhatsApp ni kuwa inaruhusu utumiaji wa kundi la watu kujiunga wakiwa na lengo maalum linalowafanya waungane katika mtandao. Hata, hivyo unapoanza kufikiria kutumia Makundi ya  WhatsApp kama chombo cha kutafuta masoko kwa bidhaa zako linaweza kuwa siyo wazo zuri.


Kwani wateja wako wanaweza kuwa na mwamko wa kupenda mazao/bidhaa  yako lakini  hawahitaji uwaunganishe na wawe wanawasiliana. Waweza kujikuta wateja wameamua kujiondoa kwenye kundi. Ni muhimu mawasiliano ya kibiashara basi yabaki ya kibinafsi kati yako na mteja.

Jinsi ya Kujitangaza bidhaa au huduma  kutumia WhatsApp

Hapa ndipo kuna mtihani mkubwa! Ni namna gani hasa itabidi kutangaza bidhaa/huduma yako kutumia WhatsApp? Kwa kuanzia unaweza kubadili picha yako ya utambulisho (profile picture)na kuweka hile haswa ya bidhaa yako. Mfano kama ni muuza maziwa basi weka picha ya mtu akimkamua Ng`ombe. Wengine uwa wanaweka logo ya kampuni badala ya picha binafsi.

Ukiweka picha ya huduma na bidhaa unayotoa inajenga umakini wa mteja kufuatilia zaidi. Baada ya hapo unaweza kuanza na kutuma picha na video za bidhaa au huduma unayozalisha kwa wateja kibinafsi kwani tayari una namba za simu zao i! Jambo lingine ni muhimu kuhakikisha kuwa kila picha na Video unayotuma inaambatana na maelezo mafupi kumfanya mteja aelewe kwa ufasaha.

Mara ngapi na muda gani kutuma Ujumbe kwa Mteja wako?

Hii tena ni muhimu sana! Huhitaji wateja wako wajifiche kwa kuwatumia ujumbe wa kujitangaza wenye maneno ya kitaalamu sana kiasi hawaelewi nini umeandika. Ukifanya hivi kitakachofuata ni wateja kuzuia wasione meseji zako tena ( blocking ).


Watumie ujumbe rahisi kuelewa  mmoja au mbili kwa wiki inatosha. Mkizoeana kwa muda sasa na wateja wako unaweza kutuma zaidi kwani wataona ni jambo la kawaida. WhatsApp kwa sasa ndio habari ya mjini linapokuja suala la Dunia ya Kidijitali. Watumiaji wa mtandao huu wanaongezeka kila siku na wanatumia muda mwingi hapa kuliko mitandao mingine ya kijamii.

Ni mtandao ambao unaunganisha watu kirahisi kwa kutumia mawasiliano ya ujumbe,picha, video na sauti. Ni rahisi kujenga mahusiano ya kibiashara na wateja wako ukitumia mtandao huu hivyo kama hujaanza kutumia tafadhali unahimizwa kuutumia na kufikisha bidhaa na huduma zako kwa wateja na kwa gharama nafuu.


Comments

Popular posts from this blog

LinkedIn: A Social Networking Site for Business People and Professionals To Connect

The Tanzania Government Invites You To Discover Some Compelling Reasons To Invest.

Investment Opportunities in Integrated Waste Management in Tanzania