Kenya 🇰🇪 Teachers Are The Most Well Paid In East Africa

Image
ANALYSIS By Dorris Otieno Kenyan teachers are not only the best paid in East Africa, but also earn almost 12 times more than the country's average pay, a comparative study by Nation Newsplex and the Institute of Economic Affairs reveals. Even as teachers go on strike for the 12th time since their first industrial action in 1962, the analysis, which compares teachers' salaries in Kenya with those of their peers in select African countries , also finds that the lowest-paid teacher in Kenya earns more than the highest-paid teacher in Uganda. Uganda and South Africa were chosen as countries against which to compare wages of teachers because they have the most up-to-date data against which the comparison could be made. While Tanzania was not included in the comparison because only average pay for the year 2011 was available, even its figures indicated that Kenyan teachers earn more than their Tanzanian counterparts. The highest paid Kenyan teacher earns almost 12 times more than the

SABABU KWA NINI UTUMIE MITANDAO YA KIJAMII KUTANGAZA BIASHARA NA SHUGHULI ZAKO





Kabla ya kukua kwa matumizi ya Intaneti, Biashara na Shughuli nyingi zilitumia mbinu ya moja kwa moja ( offline marketing tactics) kujitangaza. Kadri matumizi ya Mtandao wa Intaneti yalivyoongezeka kila mtu mwenye biashara na shughuli inayotakiwa kujulikana kwa watu alianza na kuendelea kutumia ili kuwafikia Wateja kwa Urahisi na kwa haraka sana. Tumeona Makampuni Makubwa kwa Madogo na Taasisi mbalimbali zikifungua wovuti binafsi kuwakirisha shughuli zao. Wovuti hizi zilianzishwa kiutaalamu zikisimama juu kwenye Injini za Utafutaji ( Search Engines) na Maneno Muafaka ( specific keywords).

Mfano,Daktari Bingwa wa Meno, kwenye Mtaa wa Gogo, Kariakoo angeanzisha wovuti wenye Maneno Muafaka na Maalum (specific keywords) ‘’Daktari Bingwa wa Meno, Mtaa wa Gogo ,Kariakoo’’ na kujaribu kupata webusaiti nyingine kutuma linki kweye saiti yake kusudi Injini za Utafutaji kama Google ziletee matokeo mazuri na kumweka juu ya ukurasa endapo anayetembelea mtandao wa intaneti angeandika maneno, Daktari Bingwa wa Meno, Mtaa wa Gogo Kariakoo kwa ajili ya kutafuta. Hii inajulikana kitaalamu kama ‘’SEO’’ au ‘’Search Engine Optimization.’



Kutafuta wovuti wa biashara Fulani ilikuwa haitoshi kwa watembeleaji wa mtandao (online searchers), ambao walitaka sio tu kumtafuta Daktari Bingwa wa Meno, Mtaa wa Gogo, Kariakoo, lakini kutaka kusikia pia wengine wanasema nini kuhusu Daktari huyo! Kutokana na mahitaji hayo kukaanzishwa Sehemu za Mapitio ( Review Sites) kwenye mtandao, ingawa hizi zilweza kutumiwa kiujanja na wafanyabiashara ambao walifanya kutuma Mapitio yenye kuongea vizuri juu ya biashara zao huku yakiongea vibaya juu ya Washindani wao.

 
Kutokana na hayo watumiaji wengi wa intaneti wakaanza kugeuka na kutumia Mitandao ya Kijamii ili kupata muda mzuri, habari za ukweli kuhusu taarifa za shughuli na biashara zilizopo katika maeneo yao. Hivyo, Mitandao ikajibu kwa kufanya utumiaji wake kuwa rahisi Kibiashara. Kwa kupatikana na kuunganishwa kirahisi kukaifanya mitandao ya kijamii kuwa eneo zuri kuvutia Wateja wapya katika biashara yoyote.


Kadri muda unavyoenda na kukua kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kumekuwepo na mahitaji makubwa ya Mameneja Mitandao ya Kijamii (social media managers), ambao wana Utaalamu na Nyenzo za kusaidia wenye mahitaji ya kutangaza shughuli zao kuongezeka.


Kutokana na kuwepo na watu wenye ujuzi wa kutumia Mitandao ya Kijamii, wenye Biashara wameitumia Nafasi hiyo kujitangaza zaidi na kuwafikia Wateja wao kupitia Facebook, Twitter, YouTube, LinkedIn na mingine mingi. Mitandao hii inasaidia kurahisisha mawasiliano na muungano wa manufaa kati ya WafanyaBiashara na wateja wao. 


ILANI YANGU KWAKO, Mfanyabiashara, Mwenye Viwanda, Taasisi za Kidini, Taasisi za Kibinafsi, Mashirika ya Umma, Mashirika ya Kimataifa, Wanamziki, Wanamichezo na Yeyote anayetembelea hapa na kupata habari hii ni wakati wako wa kujitangaza ili shughuli unayofanya iweze kujulikana na kuongeza kipato kwa kutumia Mitandao ya Kijamii. 


Kumbuka kuacha maoni yako au swali endapo una dukuduku lolote hapa chini na utajibiwa na wataalamu wetu.

Comments

Popular posts from this blog

LinkedIn: A Social Networking Site for Business People and Professionals To Connect

Investment Opportunities in Integrated Waste Management in Tanzania

The Tanzania Government Invites You To Discover Some Compelling Reasons To Invest.